Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo amefunga Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Jijini Arusha ambapo amewataka Viongozi kujiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao na wanapofanya maamuzi.
“Tutekeleze majukumu lakini tutoe taarifa za utekelezaji na pia tuweke mbele maslahi ya Taifa kabla ya maslahi binafsi, mlioko hapa mmeaminiwa hatuna budi kujiamini, kuamini uwezo wetu tulionao, ukijiamini utafanikiwa, usipojiamini unajiwekewea vikwazo”
“Unapofanya maamuzi sema haya ni maamuzi yangu na nimeamua haya kutokana na hili na hili na uwe tayari kusimama kutetea maamuzi yako”
“Yaliyopita sindwele tukagange yajayo, Wazungu wanasema sio kila dhoruba inakuja kuharibu maisha yako, dhoruba nyingne zinakuja kutengeneza njia kwa ajili ya maisha yako, kwahiyo madhoruba mengine tuliyowapa huko nyuma yamekuja kusafisha njia ya kwenda huko, sasa Mjengaji njia na atakayepanda juu ni wewe mwenyewe”
“Wanasema ukitaka kupanda daraja pandisha Mtu ili nawe upande daraja, usipopandisha Mtu utasimama palepale lakini ukipandisha Mtu atakuwa chini yako wewe upo juu, kwahiyo ukitaka kupanda daraja pandisha Mtu kwaza halafu panda wewe”