Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ametoa msaada kwa watu wenye uhitaji kwenye kituo cha walemavu Amani Kilichopo Chamwino Manispaa na Mission the homeless Kihonda.
Akiwakilisha msaada huo Kwa niaba ya Rais Samia ,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuwapa mahitaji muhimu wakati huu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Rc Malima amesema Serikali inawajali watu wenye uhitaji hivyo dokta Samia ameona aungane nao katika kusherekea sikukuu ya mwaka Mpya 2025
Malima amesema mpango uliopo ni kuwatambua watu wenye Mahitaji Maalum ili kuona namna ya kuwasaidia hasa wanaohitaji kwenda shule.
Aidha, Mhe. Adama Malima amesema ofisi yake itatoa ushirikiano wowote kwa lengo la kufanikisha kuwasaidia watoto hao kupata huduma muhimu zikiwemo huduma za afya, elimu na huduma nyingine muhimu zitakazowawezesha kuwajengea uwezo makundi hayo maalumu na kupata fursa za kushiriki kazi mbalimbali katika jamii ili kujikwamua na umaskini.
Walezi wa watoto hao wamemshukuru Dokta Samia kwa kuendelea kuwajali na kuwakumbuka hasa nyakati hizi za sikukuu ambapo watoto wengi wanaohitaji furaha .
“kipindi hiki Cha sikukuu watoto ndio wanakuwa wanahitaji upendo zaidi Ili nao wawe kama watoto wengine wenye wazazi hivyo msaada huu umetupa faraja”