Rais Samia ameshiriki hafla ya utiaji saini Mkataba wa Usimamizi wa Shughuli za Lishe Dodoma leo ambapo pamoja a mambo mengine amewashangaa Wakuu wa Wilaya wanaoshindwa kufanya kazi kisa kusubiri mkeka na amewaagiza Wakuu wa Mikoa wampe ripoti ya Wakuu wa Wilaya hao.
“Wakuu wa Wilaya na hii ni kwa Wilaya zote Tanzania nasikia hamfanyi kazi mnasubiri mkeka, napata mameseji
‘Malizia huku hawafanyi kazi wapo kama wamepigwa ganzi;, sasa nikute Mkuu wa Wilaya kapigwa ganzi”
“Nilisema tulichokifanya ni perfomance ya utendaji wenu, sikusema kwamba nitawabadilisha leo na kesho, nilisema tumefanva perfomance tumejua nani muri nani mbaya, aliyesema anataka kuwabadilisha nani? kama wabava nataka kuwatia kwenye mafunzo niwarekebishe?, lakini nasikia mmepigwa ganzi huko hamfanyi kazi, kwahiyo kama hamfanyi kazi hao ndio wangu”
“Wakuu wa Wilaya fanyeni kazi yenu, kutoa mkeka ni kazi yangu na nitatoa wakati napoona mwafaka, Wakuu wa Mikoa nataka ripoti za Wakuu wenu wa Wilaya, aliyepigwa ganzi nani mwenye nusu kaputi nani?, kama hawawezi tutoe tuweke wengine”