Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa matrekta matatu yenye thamani ya Tsh. 246,000,000 yenye jembe la kulimia, jembe la haro pamoja na tela katika Wilaya ya Namtumbo kwa lengo la kukuza kilimo katika Wilaya hiyo.
Rais Samia ametoa matrekta hayo kupitia Wizara ya Kilimo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amekabidhi matrekta hayo kwa Uongozi wa Wilaya ya Namtumbo na kuagiza
yapelekwe kwenye Tarafa mbalimbali, maana huko ndiko Wakulima wanatoka na amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ahakikishe matrekta yanatunzwa na kuwafikia Walengwa.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bi Ngollo Ng’waniduhu Malenya amemshukuru Rais Samia kwa kuwawezesha Wakulima kupata mbolea za ruzuku ambazo zimesababisha uzalishaji Namtumbo kuongezeka ambapo amesema dhana ya kugawa matrekta ndio dhana halisi ya Mapinduzi ya Kilimo.
Rais Samia amefikia hatua hiyo baada ya September mwaka jana, @AyoTV_ kuripoti habari ya DC Ngollo kununua na kugawa bure majembe 500 kwa Wakazi wa Wilaya hiyo kwa lengo la kuwafanya Wananchi washawishike kulima ambapo pia alisema hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua Sekta ya Kilimo Nchi huku akiwataka pia Watanzania kutolalamika kuwa ajira ngumu huku utajiri ukiwa shambani.
Vilevile trekta hizo zitatumika kulima shamba la heka 200 zilizotengwa kwa ajili ya program ya BBT Namtumbo.