Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR Samia Suluhu Hassan leo akiwa Kizimkazi Unguja ameweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa soko.
Rais Samia Suluhu Hassan kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba walikuwa kwenye tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani.
Soko hilo linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni 2 hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.