Top Stories

Rais Samia “Nisamehe kukutoa kule bila kukushirikisha” akimwambia Balozi wa Marekani

on

NI Agosti 21, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Viongozi wateule na miongoni aliowaapisha ni Elsie Sia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

“Balozi wa Marekani, Elsie Sia, nimekutoa Benki ya Dunia nimeona kazi nzuri unayofanya kule nikajua Nchi yetu ilipofika sasa na Marekani wewe ungetufaa, nisamehe kukutoa kule bila kukushirikisha, ndio uzalendo huo na nashukuru umekubali bila kuleta vikwazo”- Rais Samia

“Nchi yetu ina uhusiano mzuri na Marekani hususani wa kisiasa na uchumi, kakuze ushirikiano na uhusiano uliopo, Balozi wa Marekani unatuwakilisha pia nchini Mexico hauna budi kuingiaingia pia huko hatujaanza nao mahusiano makubwa lakini si vibaya Tanzania ikajulikana huko pia”- Rais Samia

“Balozi wa Marekani una ratibu pia shughuli za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, kwa uzoefu ulioupata kwenye Mashirika haya sina wasiwasi utatuwakilisha vizuri nina imani kubwa na wewe kwasababu umetoka huko”—Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Ikulu Dar es salaam leo

 

Soma na hizi

Tupia Comments