Rais wa Marekani Donald Trump ameanza awamu ya pili ya urais siku ya Jumatatu, wakati ulimwengu ukijiandaa na kurejea kwa kiongozi huyo asiyetabirika.
Akizungumza baada ya kula kiapo kama rais wa 47 wa Marekani siku ya Jumatatu Januari 20, 2025, ndani ya ukumbi wa Rutanda katika jengo la bunge, Rais Trump amesema ataleta mapinduzi katika maisha ya Wamarekani.
Trump aliyenusurika kutokana na mashataka ya kuondolewa madarakani, mshtaka kadhaa ya uhalifu na majaribio mawili ya kutaka kuuliwa, alipata ushindi kwa muhula mwengine katika White House, amesema atachukua hatua muhimu za kiutendaji mara tu baada ya kuapishwa.
Akimaliza sherehe za kuapishwa bungeni kiongozi huyo ataelekea katika ukumbi wa Capital One Arena ambako karibu wafuasi wake elfu 20 wamekuwa wakifuatilia sherehe na kumsubiri kumkaribisha kama rais mpya wa Marekani