Rais wa Marekani Donald Trump amekutana kwa mara ya kwanza na Baraza lake jipya la Mawaziri jana Jumatano. Ametumia mkutano huo kuelezea mafanikio yake katika udhibiti wa mpaka na mazungumzo na Urusi na Ukraine.
Trump amesema: “Tumeunda Baraza bora la Mawaziri na tumekuwa na mafanikio kabambe. Tumepewa sifa kedekede kwa kuwa na mwezi wa kwanza wenye mafanikio na tunataka kufanya hivyo kwa miezi na miaka mingi.”
Elon Musk, anayeongoza wizara mpya ya Ufanisi wa Serikali, au DOGE, alishiriki mkutano huo licha ya kutokuwa mwanachama wa baraza hilo. Alionya Marekani “itafilisika” ikiwa serikali haitapunguza matumizi.
Musk amesema: “Lengo la jumla hapa la timu ya DOGE ni kusaidia kukabiliana na nakisi kubwa. Kama nchi hatuwezi kumudu nakisi ya dola trilioni 2.”
Trump amesema anaunga mkono mpango wa Musk wa usimamishaji mkubwa wa kazi kwa waajiriwa wa serikali kuu.
Trump ameweza kupata Baraza la Mawaziri kwa haraka kuliko ilivyokuwa katika muhula wake wa kwanza, ambapo wateule 13 walishika nyadhifa zao ndani ya takribani mwezi mmoja. Katika muhula wake wa kwanza, ilimchukua zaidi ya miezi mitatu kwa mawaziri 15 kuidhinishwa na bunge la Seneti