Rais wa FIFA leo Gianni Infantino kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia 2022 kesho nchini Qatar ameongea na waandishi wa habari.
Infantino amezijia juu nchi za Magharibi kwa kukosoa Qatar kupewa uenyeji wa Kombe la Dunia kutokana na kupinga kwa baadhi ya mambo kama pombe wakidai Qatar inakiuka haki za binadamu.
Infantino ameeleza hayo huku akikemea kukosolewa vikali na nchi za Ulaya kwani ni mataifa mengi tu Ulaya yanakataza uuzwaji wa pombe viwanjani ikiwemo Ufaransa, Qatar wameruhusu pombe katika maeneo ya wazi ya kutazamia mpira na sio viwanjani.
“Nafikiri kwa vitu ambavyo sisi watu wa Ulaya tumekuwa tukivifanya kwa miaka 3000 duniani kote, tulipaswa kuomba msamaha kwa miaka 3000 ijayo kabla ya kuanza kutoa somo la maadili” >>> Infantino