Kesi ya kumuondoa madarakani Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol inafunguliwa tena Jumanne, Januari 14, mbele ya Mahakama ya Katiba ambapo mahakama inaombwa iamue iwapo itamtimua kabisa kwa jaribio lake lililofeli la kujaribu kuweka sheria ya kijeshi iliyoitumbukiza nchi hii katika mzozo mkubwa wa kisiasa.
Kikao cha kwanza cha kesi hii, kilidumu kwa dakika chache tu kwani Yoon Suk-yeol alishindwa kujitokeza.
Zaidi ya mwezi mmoja baada ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol kushindwa jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi nchini mwake, mchakato muhimu wa mahakama unaanza.
Mahakama ya Katiba ina hadi katikati ya mwezi Juni 2025 kuthibitisha au kubatilisha – hata ambayo itakuwa sawa na kumrejesha kazini kiongozi huyo – hoja iliyopitishwa Desemba 14 na Bunge la taifa, ambalo lilimsimamisha kazi Bw. Yoon.
Kesi ya kwanza ilianza saa 8 mchana kwa saa za Korea Kusini (sawa 6 saa za Ufaransa), ilichukua dakika chache tu kwani Yoon Suk-yeol hakufika, msemaji wa mahakama ameliambia shirika la habari la AFP.
Mawakili wa mwendesha mashtaka huyo wa zamani walikuwa wamesema alikusudia kuja kujieleza, lakini si leo Jumanne, wakitaja “wasiwasi kuhusu usalama na matukio yanayoweza kutokea.” Vikao vingine vinne vimepangwa katika hatua hii: tarehe 16, 21 na 23 Januari, na 4 Februari.