Top Stories

Rais wa Malawi avunja baraza lake la Mawaziri

on

Rais wa nchini Malawi, Lazarus Chakwera amelivunja baraza lake la Mawaziri  lote kutokana na masuala ya rushwa.

Akituhubia taifa lake kwa njia ya televisheni siku ya Jumatatu tarehe 24 2022, rais aliapa “kukabiliana na aina zote za uvunjaji sheria wa maafisa wa umma”.

Alisema baraza jipya la Mawaziri litatangazwa baada ya siku mbili.

Mawaziri watatu wanakabiliwa na kesi, akiwemo Waziri wa Ardhi wa nchi hio, Waziri wa Kazi, Waziri wa Nishati na wengine wakikabiliwa na kesi za rushwa.

Waziri wa Nishati alishtumiwa kuingilia mikataba ya Mafuta na pia Mawaziri hao walishtumiwa kutumia Fedha za Umma vibaya.

Wote wamekanusha madai hayo. Rais Chakwera alichaguliwa 2020, akiahidi kupambana na ufisadi.

Soma na hizi

Tupia Comments