Rais wa Marekani Joe Biden amelaani wimbi la mashambulizi ya makombora ya Urusi yaliyoua takriban watu 41 nchini Ukraine kama “kumbusho la kutisha la ukatili wa Urusi”, huku akiapa kuimarisha ulinzi wa anga wa Kyiv.
Takriban 166 walijeruhiwa kote nchini, wakiwemo wengine katika hospitali ya watoto katika mji mkuu wa Kyiv siku ya Jumatatu.
Inakuja wakati Biden anajiandaa kuandaa mkutano wa kilele wa Nato huko Washington Jumanne.
Rais wa Marekani alisema nyongeza zaidi za ulinzi wa anga za Ukraine zitatangazwa katika mkutano huo.
Viongozi kutoka mataifa 32 wanachama wa Nato, nchi washirika wao na EU wanakusanyika kuadhimisha miaka 75 ya umoja huo.
Biden alisema atakuwa akimkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na viongozi wengine wa Nato.
Mkutano huo utazingatia ulinzi na kuzuia katika muktadha wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
“Tutakuwa tukitangaza hatua mpya za kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine ili kusaidia kulinda miji yao na raia dhidi ya mashambulizi ya Urusi,” Biden alisema.
“Nitakutana na Rais Zelenskyy kuweka wazi uungaji mkono wetu kwa Ukraine hauwezi kutetereka.”