Top Stories

Rais wa Marekani Biden achoma chanjo ya tatu

on

Rais wa Marekani Joe Biden amepata chanjo ya tatu ya corona ya Pfizer ambayo imepewa jina la Booster huku akisema Watu wasiochanjwa wanaiharibu Nchi.

Chanjo ya tatu (Booster) hutolewa kwa Watu wenye umri wa miaka 65 na kuendelea na Watu wengine walio hatarini kuambukizwa Corona.

“Najua naonekana bado Kijana lakini umri wangu ni zaidi ya miaka 65 ninastahili kupata booster, wakati wengine tunachoma chanjo ya tatu kuna ambao hata chanjo moja hawajachoma sio jambo jema”

Biden amesema takribani asilimia 77 ya Wamarekani wamechanja chanjo ya corona lakini kiwango hiko hakitoshi hivyo amewataka ambao hawajachanja wakachanjwe.

R KELLY AKUTWA NA HATIA “ANAWEZA KUFUNGWA HADI KIFUNGO CHA MIAKA 10 JELA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments