Rais wa Mexico ameingia kwenye vichwa vya habari mitandaoni baada ya kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii ambayo alidai inamuonyesha mnyama mwitu ambaye sio wa kawaida (elf).
Kila kitu ni fumbo,” Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador alisema katika post yake ya Twitter Jumamosi, likiambatana na picha mbili, pamoja na moja ambayo rais anasema inaonyesha “aluxe.”
Kulingana na imani ya jadi ya jamii ya Wamaya, “aluxes” ni viumbe wadogo, wakorofi wanaoishi misituni na mashambani na huwa na tabia ya kuwachezea watu hila, kama kuficha vitu.
Obrador amepata takriban comment milioni 5 kwenye post yake kufikia Jumapili.
Picha moja kwenye chapisho inaonyesha mnyama huyo ya kabla ya Wahispania huko Ek Balam, tovuti ya Archaeolology Yucatec-Maya, wakati picha nyingine inaonyesha picha ya usiku ya kile kinachoonekana kuwa kiumbe kwenye mti na macho ya kung’aal kama mtu.
Na baada ya post hiyo wengi walisema
“haionekani rais alikuwa akitania katika post yake kwenye ukurasa wa Twitter”.
“Elf”ni aina ya kiumbe kisicho cha kawaida cha humanoid sehemu zambali za Kijerumani na Elves huonekana haswa katika hadithi za kmijerumani.
Tamaduni za enzi za kati zinazozungumza Kijerumani, elves kwa ujumla walionekana kuwa walifikiriwa kuwa viumbe wenye nguvu za kichawi na uzuri usio wa kawaida, wenye utata kwa watu wa kila siku na wenye uwezo wa kuwasaidia au kuwazuia lakini, maelezo ya imani hizi yametofautiana sana kwa wakati na nafasi na yamestawi katika tamaduni za kabla ya Ukristo na Ukristo.