Michezo

Rais wa Olympique Marseille afariki kwa corona

on

Rais wa zamani wa club ya Olympique Marseille ya Ufaransa Pape Diouf ,68, afariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, Diouf toka Jumamosi alikuwa amewekewa mashine maalum ya kusaidia mfumo wake wa upumuaji.

Pape Diouf aliyewahi kuwa Rais wa Marseille kuanzia 2005-2009 aliandika historia ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuwa Rais wa club ya soka Ulaya, enzi za uhai wake Diouf alikuwa mwandishi wa habari na wakala wa wachezaji.

Mauti yamemkuta akiwa Dakar Senegal, familia yake ilitaka asafirishwe kutoka Senegal  akatibiwe Ufaransa lakini haikuwezekana kutokana na aina ya ugonjwa aliyokuwa anaumwa.

Soma na hizi

Tupia Comments