Michezo

Rais wa PSG kwenye kashfa nzito ya rushwa

on

Rais wa club ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa Nasser Al-Khelaifi ameingia katika tuhuma za kudaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, Nasser Al-Khelaifi anahusishwa kuhusika na vitendo vya rushwa vinavyowahusisha viongozi wa wawili wa FIFA na katibu mkuu wa zamani wa FIFA katika kufanya maamuzi.

Tuhuma za Nasser Al-Khelaifi kuhusu utoaji rushwa hazijathibitika kutendeka moja kwa moja na hazihusiani na umiliki wake wa club ya PSG, Nasser Al-Khelaifi anatuhumiwa kutenda makosa hayo kama mwenyekiti wa BeIN Media Group na katibu mkuu wa zamani wa FIFA Jerome Valcke na maafisa watatu wengine kuingia katika tuhuma hizo, kuwa walifanya maamuzi kwa shinikizo.

Nasser Al-Khelaifi  inadaiwa kuwa aliwashawishi viongozi hao kinyume cha taratibu  hasa katibu mkuu Valcke hali ambayo imetia hofu ushindaji wa tenda ya haki za matangazo ya televisheni ya Kombe la Dunia (World Cup TV Right) 2026 na 2030, japo tuhuma hizo Nasser Al-Khelaifi  amezikanusha vikali na kusema kuwa hakuna kingine kimefanyika kinyume na taratibu za haki ya matangazo ya World Cup.

VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA

Soma na hizi

Tupia Comments