Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mkuu wa polisi na gavana wa benki kuu.
Tangazo lililotolewa jana usiku kwenye televisheni ya umma haikutoa sababu za kufutwa kazi kwa maafisa hao. Lilisema Kiir amemteuwa Paul Nang Majok kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi, akichukua nafasi ya Jenerali Santino Wol.
Mwishoni mwa mwezi Novemba, jaribio la kumkamata aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi lilizusha makabiliano ya risasi katika mji mkuu Juba. Mapema Oktoba, Kiir alimtimuwa Akol Koor Kuc, ambaye alikuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka wa 2011.
Alimteuwa mshirika wa karibu kiuchukua nafasi hiyo. James Alic Garang ametangazwa kuwa gavana mpya wa benki kuu, na kumrejesha Johnny Ohisa Damian kwenye wadhifa huo baada ya kumfuta kazi Oktoba 2023. Abraham Peter Manyuat ndiye Inspekta Mkuu wa Polisi akichukua nafasi ya Atem Marol Biar hii ni kwa mujibu wa DW.