Michezo

Rais wa TFF Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais mpya wa CECAFA

on

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais mpya wa baraza la vyama vya soka na vilabu vya Afrika Mashariki maarufu kwa jina la CECAFA.

Karia amechaguliwa kuwa Rais wa CECAFA katika mkutano mkuu wa CECAFA uliyofanyika leo Lugogo jijini Kampala nchini Uganda.

Nafasi hiyo Karia atadumu katika kipindi cha miaka minne akichukua nafasi ya Mutasim Gafaar kutokea Sudan aliyetawala kwa kipindi cha miaka minne katika nafasi ya Urais wa CECAFA.

Soma na hizi

Tupia Comments