Baada ya kuapishwa, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 anatarajiwa kuongoza kwa awamu nyingine ya miaka mitano baada ya kutangazwa mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo pamoja na kutangaza baraza lake na mawaziri ambalo litakuwana jukumu la kutatua changamoto za kiuchumi zinazolikabili taifa hilo.
Baada ya kuapishwa kwake leo Jumamosi, rais Erdogan anatarajiwa kuwaongoza viongozi wengine wa dunia katika sherehe katika Ikulu ya rais mjini Ankara.
Licha ya kiongozi huyo wa muda mrefu wa Uturuki kukabiliwa na changamoto za kichumi, swala la demokrasia limetajwa kuwa mojawapo ya changamoto zake haswa wakati huu kukiwa na wasiwasi na mataifa ya Magahribi.
Erdogan alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 52.2 ya kura dhidi ya mpinzani wake Kemal Kilicdaroglu aliyepata asilimia 47.8 ya kura hizo kwa mujibu ya matokeo rasimi.