Michezo

Rais wa WBF kushuhudia pambano la Mwakinyo DSM

on

Rais wa chama cha ngumi za kulipwa cha WBF Howard Goldberg atawasili nchini Jumatano kwa ajili ya usimamizi wa pambano ubingwa wa mabara super-welterweight kati ya bondia Hassan Mwakinyo na Jose Carlos Paz wa Argentina lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Oysterbay Ijumaa Novemba 13.

Goldberg atawasili pamoja na mwamuzi wapambano hilo Edward John Marshall saa 3.15 asubuhi kwa ndege ya shirikala ndege la Kenya, KQ.

Mbali ya kuwa Rais wa WBF, Goldberg enzi zake alikuwa mwamuzi na jaji wa ngumi za kulipwa duniani akiwa amecheza zaidi yapambano 300 katika nchi mbalimbali.

Goldberg anakuja nchini kwa mara ya sita kwa ajili ya kusimamia ngumi za kulipwa na amefurahishwa sana na weledi wa kampuni ya Jackson Group Sports katika pambano hili kwani wamekwisha kamilisha masharti yote ikiwa pamoja na tiketi za ndege za ujio wao.

Bondia Jose Carlos Paz (kulia) akiwasili pamoja na kocha wake, Alberto Ramon

RAIS MAGUFULI “MAWAZIRI NITABADILISHA, SIBADILISHI MA-RC WALA MA-DC FANYENI KAZI”

Soma na hizi

Tupia Comments