Rais wa Yanga SC na Rais wa Chama cha Vilabu barani Afrika (ACA) Hersi Said leo amekabidhiwa rasmi Ofisi na sasa Makao Makuu ya ACA yatakuwa nchini Morocco.
Hersi amekabidhiwa ofisi hiyo iliyoidhinishwa na CAF na Rais wa Shirikisho la soka Morocco, Fouzi Lekjaa na baada ya makabidhiano hayo, Hersi na Watendaji wengine wa ACA watafanya uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo kesho.
Awali Shirikisho la soka Afrika CAF lilikuwa limependekeza nchi za Morocco, Afrika Kusini na Kenya moja wapo ndio iwe Makao Makuu ya ACA.