Top Stories

Rais wa zamani Guinea kushtakiwa kwa mauaji

on

Mamlaka nchini Guinea zimesema kuwa zitamshtaki rais wa zamani wa nchi hiyo Alpha Conde kwa mauaji na uhalifu mwingine uliofanyika wakati wa uongozi wake.

Conde, mwenye umri wa miaka 84, alipinduliwa katika mapinduzi yaliyofanyika mwezi septemba mwaka jana.

Mwanasheria Mkuu nchini humo amesema kuwa alikuwa mmoja wa Maafisa wa ngazi ya juu zaidi ambao awali walishtakiwakwa uhalifu mkiwemo kuwafunga watu kifungo cha jela, utekeji nyara, adhabu na ubakaji.

Katika Guinea, makumi kadhaa ya wafuasi wa upinzani waliuliwa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya kupinga marekebisho ya katiba yaliyomruhusu Alpha Conde kugombea muhula wa tatu mamlakani.

Soma na hizi

Tupia Comments