Top Stories

Rais wa Zambia atumia ndege ya abiria kwenda nchini Marekani

on

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameondoka Lusaka kuelekea New York ambako atahudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la UN ambapo amesafiri kwa ndege ya abiria badala ya ndege ya Rais huku akiwa na Wasaidizi wachache.

Wazambia wamepongeza hatua hiyo wakisema inalenga kubana matumizi hasa ukizingatia kuwa Hichilema alitangaza kuwa alipoingia madarakani hivi karibuni aliikuta Hazina ya Nchi hiyo ikiwa tupu bila pesa za kutosha kuendesha Nchi.

 

WAZIRI MKUU AMBANA KWA MASWALI MAZITO AFISA WA USHIRIKA, “MNAWATOZA HELA NYINGI WANANCHI, MNAKOPA”

Tupia Comments