Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na ujumbe wake wamewasili na kupokelewa na Mhe. Ève Bazaiba, Waziri wa Mazingira wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ndjili jijini Kinshasa.
Rais Dk. Mwinyi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za kumwapisha kwa awamu ya pili Rais mteule Mhe. Félix Antoine Tshisekedi zilizofanyika katika viwanja vya michezo vya Palais du Peuple tarehe: 20 Januari 2024 jijini humo.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Lazarus Chakwera na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.