Kwa kawaida tunadhani Marais ni miongoni mwa watu wanaolipwa mishahara mikubwa sana, lakini unaweza usiamini kuwa kuna baadhi ya nchi zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi lakini Marais kutoka nchi hizo bado wanalipwa mishahara midogo.
Leo May 1, 2017 nimekusogezea list ya Marais watano ambao wanatajwa kulipwa mshahara mdogo zaidi duniani na rekodi yao haijawahi kuvunjwa hadi kufikia 2017.
1: Xi Jinping
Licha ya China kuwa miongoni mwa nchi zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi duniani, lakini Rais wa nchi hiyo anatajwa kuwa miongoni mwa Marais wanaolipwa mshahara mdogo ukilinganisha na marais wa mataifa makubwa. Xi Jinping anatajwa kulipwa mshahara wa Dollar 1,120 kwa mwezi.
2: Jose Mujica
Jose Mujica alikuwa Rais wa Uruguay kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, lakini bado anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa Rais namba mbili anayelipwa mshahara mdogo zaidi duniani. Jose Mujica alikuwa analipwa Dollar 1,250 kwa mwezi.
3: Macky Sall
Huyu ni Rais wa Senegal wa sasa, alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012 na anatajwa kushika namba tatu kwenye list ya Marais wanaolipwa mshahara mdogo zaidi duniani akilipwa Dollar 1,300 kwa mwezi ambayo ni sawa na Dollar 15,600 kwa mwaka.
4: Beji Caid Essebsi
Beji Caid ni Rais wa sasa wa Tunisia ambaye alichaguliwa December 2014. Beji anatajwa pia kuwa miongoni mwa Marais wanaolipwa mshahara mdogo zaidi duniani ambapo analipwa Dollar 1,350 kwa mwezi.
5: Pranab Mukherjee
Alichaguliwa kuwa Rais wa India July 2012 na anatajwa kuwa miongoni mwa Marais wanaolipwa mishahara midogo zaidi duniani akishika namba tano. Pranab Mukjerjee anatajwa kulipwa Dollar 2,400 kwa mwezi.
VIDEO: Ulipitwa na hili agizo alilolitoa Rais Magufuli Kilimanjaro? Bonyeza play kutazama…
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo