Mix

Raisi wa Barca ataka Messi amzidi Ronaldo na kuwa mwanasoka anayelipwa zaidi duniani

on

140127155621_messi__512x288_afp

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hauzwi na klabu hiyo inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina, amesema rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.

Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d’Or, mwenye umri wa miaka 26, anatakiwa na matajiri wa klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain.

Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1, yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema: “Klabu itakaa na kuangalia mkataba mpya. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi duniani.”

Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50 aliyocheza msimu uliopita na hadi sasa amefunga mabao 18 na manane kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi.

Tupia Comments