AyoTV

Rais Magufuli alivyoagiza mil. 200 za sherehe ya Wabunge zipelekwe Muhimbili.. (Video)

on

Hii stori ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii, wapo walioamini na wapo walioona kama huo ni ujumbe wa uzushi… wakati unavyozidi kusogea ukweli umezidi kuthibitika kwamba haikuwa uzushi, agizo hilo limetolewa na Rais Magufuli mwenyewe !!

Nakusogezea uthibitisho mwingine kutoka Ikulu, hii ni nukuu ya alichokisema Rais Magufuli kuhusu agizo hilo >>> “Nitaomba mnisamehe sana, inawezekana sherehe ya leo isiwe nzuri kama mlivyozoea, hakuna bia… inawezekana kama kuna chupa za wine ni chache, mengi ni maji na soda.”

Sentensi zake nyingine hizi hapa >>> “Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda“- Dk. J.P Magufuli.

Video yake hii hapa kwenye dakika mbili.

Lakini hili agizo liliwekwa pia kwenye Website ya Ikulu jana hiyohiyo.

IKULU

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments