Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Huyu ndio Rais wa nchi anaecheza mpira wa kulipwa cheki na mshahara wake hapa.

on

prezdaaNikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wa nchi kwenye hili soka unaweza kuotea? hii inaingia kwenye list ya stori kubwa za millardayo.com

prezzzSasa unaambiwa club moja huko Bolivia (Sports Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti 2014 na mgongoni atakua na jezi namba 10 huku mshahara wake kwa mwezi ukiwa ni dola za Kimarekani 213 kwa mwezi ambazo ni zaidi ya laki 3 za Kitanzania.

prezKwa sasa mashabiki wanamsubiri president huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae ni shabiki mzuriย  soka na atakua akiichezea Sports Boys ikiwa ni timu iliyopo kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.

Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mechi watakayokuwa wanacheza hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.

Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine huku kumbukumbu ikionyesha mwaka 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekwa kwa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa.

Mwaka 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa.

Kama unataka stori kama hizi zisikupite ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila stori inayonifikia.

Tupia Comments