Ilikuwa kujaribu bahati ya mara ya sita kwa Hakainde Hichilema, ambaye hatimaye amekuwa rais wa Zambia baada ya majaribio matano yasiyofanikiwa.
Bwana Hichilema alimshinda mpinzani wake mkuu, Rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, kwa zaidi ya kura milioni.
Bwana Hichilema, 59, amejielezea kama “kijana wa kawaida”, ambaye alichunga mifugo ya familia yake katika ujana wake kabla ya kuwa mmoja wa watu tajiri zaidi nchini Zambia.
Stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.