Michezo

Raja Casablanca wawakosa watu 6 muhimu kikosini

on

Club ya Raja Casablanca ya Morocco leo imesafiri kuelekea Cairo Misri kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek.

Raja katika safari hiyo imewaacha golikipa Anas Zniti, beki Abdelilah Jbira, kiungo Mohamed Douik, fitness trainer, Doctor na Physiotherapist sababu yadaiwa kuwa hofu ya Corona.

Awali wizara ya afya Morocco ilipelekea CAF kuahirisha mchezo huo baada ya kuagiza kikosi kizima cha Raja kukaa karantini walau wiki moja kujisikilia hali zao na sasa mchezo utachezwa Novemba 4 2020.

Soma na hizi

Tupia Comments