Hivi karibuni tulipata taarifa za madai kutoka katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuhusu hoteli yetu, Ramada Resort Dar es Salaam.
Ramada Resort Dar es Salaam inapenda kuufahamisha umma kwamba inazingatia kanuni na maadili ambazo zinaambatana na viwango vya Tanzania na vya kimataifa.
Shughuli zetu zinazingatia kikamilifu sheria na kanuni za Tanzania, huku tukihakikisha kuwa kazi zetu zote ni halali na zina zinaheshimu jamii *inayotuzunguka. Hii inajumuisha kutoa maagizo kwa wageni wote kujisajili mara tu wanapowasili na kutoa vitambulisho
halali.
Hatua hizi zimewekwa ili kuhakikisha kunakuwa na usalama, ulinzi na faragha kwa wageni
wetu wote.
Tumefahamishwa kwamba kuna barua batili imesambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya
kijamii, ikihusisha kimakosa hoteli yetu na shirika/jumuiya ya LGBTQ.
Shirika lililotajwa katika barua hiyo limetoa taarifa kwa umma inayothibitisha kuwa barua hiyo ni ya kughushi na batili na halikuhusika kuitoa.
Tunathibitisha kwa dhati kuwa* hatuna uhusiano wowote na shirika lililotajwa katika barua
hiyo na hatujawahi kuhusishwa au kupokea msaada wa kifedha kutoka kwenye shirika hili, au kikundi kingine chochote kinachohusiana nalo.
Uchunguzi wa ndani umegundua kwamba madai haya ya kuhusisha Ramada Resort Dar es Salaam na shirika la LGBTQ ni ya uwongo.
Pia, tunaendelea kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha kuwa suala hili
linashughulikiwa vizuri.
Tumejizatiti kuweka mazingira mazuri ya kuheshimika kwa wageni wote, yanayozingatia
sheria, maadili na utamaduni wa Tanzania katika juhudi za kuchangia kuinua sekta ya utalii ya nchi yetu kwa faida ya Umma.
Tunawaomba wananchi kuipuuza habari hio inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.