Michezo

Baada ya Madrid kuikataa Ofa ya Man Utd, Ramos amefanya uamuzi huu

on

Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye yupo mapumzikoni ametoa kauli yake.
United walituma ofa ya kwanza ya paundi milioni 28.3 kwa Madrid ili kupata saini ya beki huyo wa kimataifa wa Spain, lakini Madrid waliikataa ofa hiyo.

Hata hivyo baada ya Ramos kugundua Madrid wameikataa ofa hiyo, alichukua uamuzi wa kuwaweka wazi viongozi wa Madrid kupitia wakala wake kwamba anataka kuondoka na kujiunga na United na kuiomba Madrid ikubaliane bei na Manchester United.

Uamuzi huo wa Ramos umeishtua Madrid, ambao walitegemea wangefanya makubaliano ya mkataba mpya na beki huyo.

Madrid wanategemewa kujaribu kumtuliza Ramos na mkataba mnono mpya lakini kaka na meneja wa mchezaji huyo, Rene Ramos ameshaifahamisha Madrid lengo la mteja wake kutaka kuanza maisha mpya sehemu nyingine.

Rene ameripotiwa kusema kwamba Ramos anataka kuhamia Old Trafford wakati huu wa dirisha la usajili na klabu pekee ambayo anataka Madrid ifanye nayo makubaliano ni United.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments