Michezo

Ramos asaini PSG 2023

on

Aliyekuwa beki wa Real Madrid Sergio Ramos (35) amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia PSG ya nchini Ufaransa, Ramos amesaini kama mchezaji huru.

Ramos anajiunga na PSG baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Real Madrid ambapo Ramos aliomba mkataba wa miaka miwili wakati Real Madrid wakitaka kumpa mkataba wa mwaka mmoja kabla ya baadae kufuta mpango huo kabisa.

Sasa Ramos atakuwa PSG hadi June 30 2023, akicheza kwa miaka 16 Real Madrid, Ramos amecheza mechi 671 na kafunga magoli 101 katika kipindi cha kati ya 2015-2021 Ramos ameisaidia Real Madrid kushinda Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne.

Soma na hizi

Tupia Comments