Mix

Rannia Nasser aja na maonesho ya picha maarufu kama “Watu Wa Tanzania”

on

Mwanafunzi wa sekondari umri wa miaka 17 Rannia Nasser ameandaa maonesho ya picha maarufu kama
‘WATU WA TANZANIA” yatakayofanyika katika ukumbi wa Alliance Francie na kudhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa siku tano mfululizo kuanzi tareh 7 hadi 12 mwezi huu.
Lengo ikiwa ni kusaidia kusaidiana kukuza utalii nchini kutokana na picha hizo kubeba maudhui yanayoonesha shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na maisha halisi ya mtanzania yaliyojaa simulizi na historia za Taifa letu.

Akizindua maonesho hayo rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nje Dr Damas Ndumbaro  kwa niaba ya Serikali ya Tanzania aliahidi kuendelea kuimarisha mahusiano ya Kidemokrasia na kiuchumi kati yake na Serikali ya Ufaransa ikiwa ni pamoja na kutumia mahusiano hayo katika kuitangaza Sekta ya utalii iliyopo nchini ili sekta hiyo iweze kutangazika zaidi katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Amesema “Tanzania na Ufaransa tunamahusiano mazuri kwa muda mrefu hali ambayo kwa kiasi kikubwa inatunufaisha nchi zote kwenye nyanja mbalimbali hivyo ni wajibu wetu kama nchi kuyatunza mahusiano haya ili yanendelee kutunufaisha”.

Pia mara Baada ya kuzindua Maonesho hayo Dokta Ndumbaro alipongeza  mwanafunzi Rannia Nasser kwa jinsi alivyojitoa muda wake na kupiga picha nzuri zinazoonesha uhalisia na jinsi watanzania tunavyoishi kwa upendo Amani na kuamua kuzitoa bure picha zote kwa Bodi ya Utalii Tanzania ili zitumike kukuza utalii nchni “Hongera Rasana Rannia kwa niaba ya watanzania wote ninakushukuru” DR Damas Ndumbaro

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier kwa nafasi yake pamoja na mambo mengine ameahidi kuendelea kuzitangaza fursa za utalii zilizopo Tanzania ili sekta hizo ziendeleee kuiamrika na hatimaye kukuza uchumi wa Taifa.

“Sisi Ufaransa tutaendelea kushirikiana na Tanzania ili kila ubunifu unaolenga kuimarisha utalii uweze kuleta maendeleo nchini.” >>> Frederic Clavier

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi  akiahidi kuziweka picha hizo katika vivutie vya utalii nchini livyopo nchini na kubanisha kuwa sanaa  hii  ya picha  ambayo imepewa jina la Watu wa TANZANIA wataiendeleza kwa kuwa itasaidia mataifa mengi ulimwenguni kufahamu uhalisia wa maisha ya watanzania vyema na kukuza Utalii

Soma na hizi

Tupia Comments