Duniani

Hii ndio Hospitali ya kwanza kufunguliwa kitengo cha kuhudumia Wanaume waliobakwa !!

on

Kesi za wanawake kubakwa au kudharirishwa kijinsia ni kitu ambacho kimesikika sana.. lakini ishu za matukio ya wanaume kubakwa sio stori ambazo zimesikika sana au kuzoeleka masikioni mwa wengi !!

Hii Hospitali imeangalia pia umuhimu wa kutoa huduma kwa wanaume ambao wamebakwa au kufanyiwa ukatili wa kijinsia, ni Hospitali ya Södersjukhuset ambayo iko Jiji la Stockholm, ndani ya Sweden.

Uongozi wa Hospitali hiyo wameweka Kitengo cha Huduma ya Dharura kwa ajili ya kuhudumia Wanaume waliobakwa, Huduma kwenye Hospitali hiyo zinatolewa kwa saa 24 na kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili…

mg_sadman_comp

Mmoja wa Viongozi wa Serikali alielezea umuhimu wa Huduma hiyo >>>>”Nadhani hii ni Kliniki ya kwanza Duniani, tumefanya Utafiti Mitandaoni na hatujaona kama kuna sehemu nyingine inatoa Huduma ya aina hiyo… Wanaume wote watahudumiwa bure kabisa… Ni matumaini yetu kwamba waathirika wengi wa matukio ya aina hiyo ambao huwa wanajificha, watajitokeza kuhudumiwa

Huduma hii inaonekana kuwa na umuhimu wake kwa Wanaume wa Sweden, Takwimu zinaonesha kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2010 Sweden iliongoza kwenye Takwimu za matukio ya Wanaume kubakwa katika Nchi za Ulaya.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments