Habari za Mastaa

Rapper Bilionea Jay Z atimiza miaka 50

on

Rapper Jay Z ametimiza umri wa miaka 50 leo, ana rekodi ya kushinda Tuzo 22 za GRAMMY, yupo kwenye 100 bora ya Wasanii bora wa dunia kwa mujibu wa billboard, pia ni Bilionea Mwana-Hiphop wa kwanza.

Anashikilia pia rekodi ya kuwa Muamerika mweusi namba tatu kwa utajiri, Yeye na Ndugu zake Watatu walilelewa na Mama yao baada ya Baba kuitelekeza familia.

Jigga ambae aliwahi kuja Tanzania mwaka 2006, aliwahi kumpiga risasi ya bega Kaka yake kutokana na kumuibia vito vya thamani. 

NDANI YA MAHAKAMA WAMETAZAMA VIDEO YA ZITTO KABWE MWANZO MWISHO

 

Soma na hizi

Tupia Comments