Habari za Mastaa

Rapper wa Marekani apigwa risasi nyumbani kwake na kufa

on

Rapa chipukizi kutokea Marekani Pop Smoke ameripotiwa kuuwawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mjini Hollywood Hills

Taarifa zinaeleza kuwa Pop Smoke mwenye umri wa miaka 20, alivamiwa nyumbani kwake majira ya saa 10 usiku na wanaume wawili waliokua wamejifunika nyuso zao wakiwa ndani ya makoti yenye kofia zinazofunika kichwa na kumpiga risasi rappa.

Baada ya tukio hilo rapa huyo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Cedar-Sinai Medical Center huko magharibi mwa Hollywood ambapo baadae ilitangazwa kuwa amefariki Dunia.

Kama utakumbuka Pop Smoke ameshawahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo kufanya wimbo na Nicki Minaj pamoja na Travis Scott, na alikuwa akipewa nafasi ya wasanii wanaofanya vizuri Kwenye muziki.

 

Soma na hizi

Tupia Comments