Top Stories

Rasmi Biden ndie Rais wa 46 wa Marekani, atoa hotuba nzito

on

“Hii ni siku ya Wamarekani. Hii ni siku ya demokrasia. Siku ya historia na matumaini.” Ni kauli ya Rais Joe Biden baada ya kula kiapo.

Rais Joe Biden ametoa wito kwa Wamarekani wote kuheshimiana katika jamii zao na kuongeza kuwa Umoja wao ni muhimu kwaajili ya kuifanya Marekani iliyo bora zaidi.

Amesema hayo mara baada ya kula kiapo mbele ya wageni waalikwa na viongozi mbalimbali waandamizi na wastaafu katika sherehe za kula kiapo zilizofanyika jijini Washington DC na kusema kuwa, pasipo na Umoja hakuna Amani.

“Acheni kupiga kelele na shusheni joto la hasira lililopo miongoni mwetu, Umoja ni njia ya kusonga mbele,” Rais Biden.

Joe Biden ameapa kuwa Rais wa Marekani wa 46 kwa kushika Katiba ya Nchi hiyo akiongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu, John Roberts na kushuhudiwa na mkewe Dkt. Jill Biden.

TAZAMA TRUMP ALIVYOONDOKA WHITE HOUSE NA HELIKOPTA NA KUAHIDI ATARUDI KWA NJIA NYINGINE

Soma na hizi

Tupia Comments