Habari za Mastaa

Usher Raymond kafunga ndoa kimyakimya? Nyepesi nyepesi ni hizi toka Cuba..

on

Msanii wa R&B Marekani Usher Raymond amekuwa mtu wa kimya kimya sana siku hizi, yani mambo yake mengi anafanya kwa kushitukiza, pengine hii ndio style yake mpya ya maisha, kufanya mambo chini chini bila kuongea sana mitandaoni!

usher4

Usher Raymond.

Nimekutana na stori kwenye mtandao wa Us Weekly wa Marekani ambao wenyewe umeweka wazi siri ambayo msanii wa R&B Usher Raymond amekuwa akijaribu kuficha kwa muda wa wiki sasa… wamenasa picha kutoka kwenye Instagram ya Grace Miguel ambaye taarifa ikufikie mtu wangu ni mke wa sasa wa Usher Raymond!

uuuussh2

Usher Raymond & mke wake wa sasa Grace Miguel.

Wawili hao waliamua kufunga ndoa ya kisiri siri baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka mitano na kwa mujibu wa mtandao wa Us Weekly wawili hao walifunga ndoa hiyo mwanzoni mwa mwezi September.

usher2

Grace Miguel pia ni manager wa Usher Raymond mtu wangu!

Honeymoon yao ilikuwa huko Havana, Cuba na walipanga sherehe simple ya wageni 100 lakini badaae wawili hao wakabadilisha mawazo na kuamua kufanya kitu kingine kabisa, waliamua kutoroka kwenda sehemu ya mbali kimya kimya na kufunga ndoa hiyo… licha ya kuwa mke mpya wa Usher Raymond, Grace Miguel pia ni Manager wa Usher!

uuushhh

Picha kutoka kwenye page ya Instagram ya Grace Miguel mke wa sasa wa Usher Raymond… wenyewe hapa walikuwa Cuba wakienjoy honeymoon yao!

Usher hajazaa mtoto yoyote na Grace Miguel toka waanze uhusiano yao mwaka 2009 ila wawili hao wameweka wazi kuwa wanategemea kujipanga kwa ajili ya mpango huo hivi karibuni… Usher ana watoto wawili kutoka kwenye ndoa yake ya mwanzo na Tameka Foster; Naviyd Ely mwenye miaka 6 na Usher Raymond V mwenye miaka 7.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments