Top Stories

RC aagiza Watumishi 34 kuwekwa ndani kwa ubadhirifu wa Milioni 307 (+video)

on

Mkuu wa Mkoa Kagera Brig.Jen. Marco Gaguti amemuagiza kamanda wa polisi mkoani humo pamoja na Kamanda wa TAKUKURU kuwakamata watumishi 34 katika Halmashauri ya wilaya Biharamulo wakiwemo Watendaji wa Vijiji na Kata kwa kushindwa kurejesha fedha shiligi Milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa Benki.

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku 7 lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia 2%, kwa mwendo huu hatuwezi kwenda lazima tuweke misingi imara ya kuboresha utumishi na uadilifu” Gaguti

“hapa nina orodha ya watendaji 30 ambao nampatia kamanda wa polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wanne hawa naagiza wasimamishwe kazi lakini wawe chini ya uangalizi wa kamati ya ulizi na usalama ili kutoa ushirikiano” Gaguti.

MAGUFULI “IGP SIRRO USIJIDANGANYE KUGOMBEA UBUNGE, NITAKUFUTA HATA UKISHINDA”

Soma na hizi

Tupia Comments