Top Stories

RC Arusha aibuka na Machinga “Tutawapanga, inatumika kama siasa” (video+)

on

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema watashirikiana na wafanyabiashara na wadau wengine ili kuweza kuwapanga wamachinga huku akionya wanaopotosha nakutumia jambo hilo kama siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari alisema..“Alipokuwa akiwaapisha Mawaziri na Mwanasheria Mkuu, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kwamba wamachinga wapangwe kwani kuna wamachinga wengine wanapanga biashara zao mbele ya makazi ya walipa kodi”- RC Arusha

“Sisi kama mkoa tumeshaanza kutizama mifumo yetu na jinsi gani tutafanya hivyo, tutawashirikisha hata viongozi wadogo wadogo, tutasimamia haki na sheria hususani maagizo ya Mheshimiwa Rais”- RC Arusha
Ayo TV & Millardayo.com imekuandalia hapa habari kamili unaweza ukabonyeza play kutazama.

JANETH AKAMATWA KWA KUMCHOMA MTOTO WAKE MOTO KISA KUOMBA HELA

Tupia Comments