Top Stories

RC Chalamila awapa onyo kali waliosamehewa “mtawasahau ndugu zenu” (+video)

on

Serikali imeahidi kuwasaidia kiuchumi wafungwa 259 waliotoka kwenye Magereza ya Mkoa wa Mbeya na Mikoa mingine kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alioutangaza jana kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru.

RC Mbeya Albert Chalamila ameyasema hayo wakati wa zoezi la kutoka gerezani wafungwa hao kwenye Gereza la kilimo la Songwe na kufahamisha kuwa wanafanya utaratibu watu hao waliopata msamaha wa Rais wafike kwenye kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya wanakotoka na kujiorodhesha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuendesha maisha yao baada ya kutoka kifungoni.

Kwa upande wao wafungwa waliopata msamaha wa Rais wameeleza kuwa watakuwa raia wema kwenye jamii kwa kujutia makosa yao.

RC MWANRI ATAMANI KUTUMIA HELIKOPTA KWENYE KILIMO “TUTAZALISHA TANI 15,000”

Soma na hizi

Tupia Comments