RC Chalamila na Makampuni yajitokeza kununua tiketi kuelekea mchezo wa Yanga SC dhidi ya USM Alger
Share
2 Min Read
SHARE
NI Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ambae leo Mei 24 ,2023 ameunga mkono hamasa ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua tiketi 𝟭𝟬𝟬𝟬 za mchezo wetu wa fainali #cafcc dhidi ya USM Alger Jumapili.
Aidha RC Chalamila akiongea na waandishi ofisini kwake alisema..“Nina furaha kubwa sana kwa namna Young Africans SC ilivyotupa heshima na ninamshukuru sana kwa dhati Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza hamasa hii kubwa sana kwenye michezo tena kwa vitendo”
Mbali na ungwaji wa RC Chalamila katika ununuzi wa tiketi hizo pia zipo Makampuni binafsi na watu waliojitokeza kuunga Mkono hamasa ya Rais Samia Suluhu Hassan juu ya ununuzi wa tiketi za mchezo wa Yanga SC dhidi ya USM Alger ambapo mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jumapili hii.
.Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank amuunga mkono Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hamasa ya mchezo wetu wa fainali ya kwanza #CAFCC kwa kununua tiketi 𝟱𝟬𝟬𝟬..Ruth Zaipuna ambae ni Afisa Mtendaji Mkuu NMB amuunga mkono Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hamasa ya mchezo wetu wa fainali ya kwanza #CAFCC kwa kununua tiketi 𝟱𝟬𝟬𝟬......Al-watan Hamza Kaimu Mwenyekiti Yanga Whatsapp Makao Mkuu pongezi kwake kwa kununua tiketi 𝟭𝟬𝟬 za mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho #CAFCC dhidi ya USM Alger utakaopigwa Jumapili ya tarehe 28.05.2023, Saa 10:00 Jioni kwenye Dimba la Benjamin Mkapa...Pichani: Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC amuunga mkono Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hamasa ya mchezo wetu wa fainali ya kwanza #CAFCC kwa kununua tiketi 𝟱𝟬𝟬𝟬.