Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: RC Makalla aagiza kufunguliwa kwa BAR na Hoteli Zilizofungwa na NEMC Mwanza
Share
Notification Show More
Latest News
Habari kubwa Magazetini Kenya leo June 4, 2023
June 4, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 4, 2023
June 4, 2023
Picha: Kutoka Airport DSM, Ndege ya kwanza ya mizigo ‘Boeing 767-300F ilivyotua, Rais ashuhudia
June 3, 2023
Mapokezi ya ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F
June 3, 2023
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuapishwa kuliongoza taifa hilo
June 3, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > RC Makalla aagiza kufunguliwa kwa BAR na Hoteli Zilizofungwa na NEMC Mwanza
Top Stories

RC Makalla aagiza kufunguliwa kwa BAR na Hoteli Zilizofungwa na NEMC Mwanza

May 26, 2023
Share
3 Min Read
SHARE

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla ameagiza kufunguliwa kwa Bar na Hotel zote zilizofungiwa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa kosa la kufungulia muziki mkubwa na kuweka utaratibu wa haraka wa kuelimisha makundi hayo.

Mhe. Makalla ametoa agizo hilo mapema leo ijumaa Mei 26, 2023 wakati wa kikao chake na wamiliki na wafanyabiashara wa Bar na hotel mkaoni humo kilichifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

“Bar na hoteli hizi zikisimama, ajira zitasimama, biashara zitasimama na uchumi utasimama na tujiulize watawezaje kulipa faini wanazodaiwa wakati biashara wamefunga hawafanyi tena.” Amesisitiza Makalla.

RC Makalla amepiga pia marufuku ukamataji wa nguvu huku akibainisha kuwa wafanyabiashara hao sio majambazi hivyo wanapaswa kuelimishwa wanapokosea kwa kuangalia uhalisia wa maisha kwani kuua biashara ni rahisi sana kuliko kuijenga.

Aidha RC Makalla amewataka NEMC na wafanyabiashara waliopigwa faini kuketi pamoja na kuzungumza namna ya kumaliza matatizo hayo ili kuhakikisha biashara hazisimami kwa sasa na amewataka watulie na kuondoa hofu kutokana na tafrani za kamata kamata.

“Nataka NEMC watoke kwenye kuwa taasisi ya kamata kamata na kuwa kama chuo kwa kuwaona wadau wao kama watoto na wao kuwa walezi na wajikite kwenye kutoa elimu ili watambue nini wanapaswa kufanya na kitu gani hawapaswi kufanya.”–RC Makalla.

.

Akisoma risala kwa niaba ya wafanyabiashara hao, Richard Lomweti amesema operesheni inayofanywa na NEMC kwenye Bar na kumbi za starehe kuanzia Mwezi Mei 2023 imewaumiza kwa kuwapiga faini kubwa kwa kudai kuwa wanazalisha kelele tena bila kutoa elimu kwao hususani wakati wa kutoa leseni.

“Kifaa wanachotumia NEMC kinaonekana hakina uhalisia wa vipimo kwani hata muziki ukizimwa kinaonesha muziki umezidi kiwango na pia kinahusisha hata kelele zingine nje ya muziki husika kuwa ni kelele za muzuki.” Amesema bwana Lomweti.

Aidha, amefafanua kuwa faini wanazotozwa na NEMC pamoja na adhabu za kuwekwa ndani au kizuizini zimekuwa kubwa tofauti na uhalisia wa kosa hivyo wametoa wito kwa taasisi hiyo kuondoa faini hizo zinazowaumiza kiuchumi.

Vilevile, wameomba NEMC kuketi nao kwa pamoja kuzungumza na kuona namna ya kuboresha huduma hizo pasipo kubughuzi na kwamba wafute faini zote na kufuta sheria kandamizi zisizoendana na mazingira halisi ya uchumi wa sasa.

.

You Might Also Like

Picha: Kutoka Airport DSM, Ndege ya kwanza ya mizigo ‘Boeing 767-300F ilivyotua, Rais ashuhudia

Mapokezi ya ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuapishwa kuliongoza taifa hilo

Watu 288 sasa wamethibitishwa kufarikiwengine 900 kujeruhiwa katika ajali ya treni India

Ukraine iko tayari kuzindua mashambulizi-Volodymyr Zelensky

Edwin TZA May 26, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Festo Sanga amwambia Waziri Mabula, ‘Utaondoka kwenye wizara hii, okoa mauji yanaendelea Tanzania’
Next Article GSM Group imejumuika na Mabalozi, Viongozi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Afrika Duniani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Habari kubwa Magazetini Kenya leo June 4, 2023
Magazeti June 4, 2023
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 4, 2023
Magazeti June 4, 2023
Picha: Kutoka Airport DSM, Ndege ya kwanza ya mizigo ‘Boeing 767-300F ilivyotua, Rais ashuhudia
Top Stories June 3, 2023
Mapokezi ya ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F
Top Stories June 3, 2023

You Might also Like

Top Stories

Picha: Kutoka Airport DSM, Ndege ya kwanza ya mizigo ‘Boeing 767-300F ilivyotua, Rais ashuhudia

June 3, 2023
Top Stories

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuapishwa kuliongoza taifa hilo

June 3, 2023
Top Stories

Watu 288 sasa wamethibitishwa kufarikiwengine 900 kujeruhiwa katika ajali ya treni India

June 3, 2023
Top Stories

Ukraine iko tayari kuzindua mashambulizi-Volodymyr Zelensky

June 3, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?