Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameomba wananchi kuendelea kuomba ili mvua zinyeshe kusaidia uzalishaji wa maji safi na salama ambao kwa sasa umepungua kwa zaidi ya lita milioni 70 kwa siku licha ya juhudi za kusafisha wavamizi katika bode la mto Ruvu.
“Hali sio nzuri maji yamepungua sana, Rais alitoa maelekezo na Waziri Mkuu alifika maeneo na kuagiza kufanyika oparesheni na utekelezaji umeenda vizuri, chanzo cha maji haya ni mvua na hapa tulikua tunatarajia mvua za vuli zinazoaanza mwezi October, November miezi yote hii haijanyesha, ndio ambayo ingerekebisha hali, upungufu wa maji ni lita Milioni 70 kila siku” RC Makalla
“Kibinadamu tumefanya yaliyobaki ya KIMUNGU, mvua ndio chanzo, hata huko Milima ya Uruguru hamna mvua watu wameshindwa kulima hamna mahindi, na sio katika maji hata kwenye mabwawa ya umeme yanakauka na yote vyanzo ni mvua ni maji ni UKAME” RC Makalla
Akizungumza baada ya kutembelea vyanzo vya maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu, Makalla ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji amesema kwa sasa maji yanayo zalishwa ni lita milioni 200 na kwamba mgao wa maji utaendelea kuwepo kwa muda mrefu.
Mahitaji ya Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Lita Milioni 520 kwa siku.