Top Stories

Makonda akikabidhi ofisi “mbwa mwitu wakawa wanabweka

on

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda leo August 3, 2020 amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huo wa sasa Aboubakar Kunenge, ambapo amesema amehitimisha safari yake ya ukuu wa mkoa.

Makonda amesema Rais Magufuli alimuamini na kuamini anachokifanya ndio maana aliibuka kidedea kudhibiti madawa ya kulevya katika mkoa huo.

“Rais aliniamini na kuamini ninachofanya ni kwa faida ya Watanzania na tukaibuka kidedea dhidi ya mapambano ya Dawa za Kulevya, JPM ni Rais msikivu kwangu tena mnyenyekevu na Mcha Mungu ambaye daima nitaendelea kumuenzi kwa vitendo” Makonda

“Rais Magufuli aliamini katika Vijana nikiwa Kijana wa kwanza kupewa majukumu katika Mkoa mkubwa na kuacha alama itakayodumu milele, namshukuru JPM kwa mambo mengi ikiwemo uvumilivu wake” Makonda

Ukiteuliwa unaanza kufanya kazi, kazi unayofanya inaweza kuleta kelele na mbwa mwitu wengi wakawa wanabweka lakini Rais wetu aliziba masikio akaendela kuniamini na Tarehe 15 nimeondoka mwenyewe ikiwa ni ishara ya kukubali kazi niliyofanya na kuamini ya kwamba sasa umefika wakati uende kwenye majukumu mengine” Makonda

Soma na hizi

Tupia Comments