Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkoa wa Njombe imebaini nyumba chakavu katika Mtaa wa Ramadhani, mjini Njombe inayodaiwa kutumiwa na mfanyabiashara mmoja (jina limehifadhiwa), kuchakachua mbolea va ruzuku.
Ndani ya nyumba hiyo zilikutwa shehena ya mifuko ya mbolea za ruzuku aina mbalimbali zikiwamo Urea, Can na OCP na mifuko mitupu, mashine moja ya kushonea pamoja na majenereta mawill.
Imedaiwa kuwa nyumba hiyo inatumika kufanya udanganyifu wa kuchanganya mbolea hizo kisha kuuzwa kwa wakulima.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka, alisema kamati hiyo ilibaini tukio hilo Januari 17, mwaka huu majira ya saa nne usiku baada va kupata taarifa za siri.