Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Januari 16, 2025 Ofisini kwake amempokea na kufanya kikao kifupi na Balozi Mhe. Marianne Young, Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania ambapo Mhe. Young yupokwenye ziara ya kikazi Mkoani Mwanza katika Wilaya za Ilemela, Nyamagana na Magu.
Mhe. Mtanda amesema Tanzania na Uingereza wamekuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia kwa kipindi kirefu ambapo wamekuwa wakisaidiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo miradi ya sekta ya Afya, elimu pamoja na miundombinu.
Naye Mhe. Balozi Young amemshukuru Mhe. Mtanda kwa ukaribisho mzuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano kadhalika amemualika Mkuu huyo wa Mkoa, Makao Makuu ya Ubalozini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo ya kimkakati.