Mkuu wa Mkoa Morogoro Fatma Mwasa amezitaka taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kilimo kutoa elimu kwa wakulima ili wananchi wajikwamue kupitia sekta hiyo.
RC Mwassa ameyasema hayo wakati akifunga tamasha la kilimo Marathon lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Manispaa ya Morogoro.
Mwassa amesema taasisi zinatanakiwa kufanya kazi ya kuelimisha wakulima huku akiiipongeza taasisi ya TAHA kwa kuibuka kidedea kama Taasisi ya binafsi yenye mchango mkubwa kwa wakulima katika kuwapatia elimu ya Kilimo bora na kupata Tuzo katika tamasha Hilo la Kilimo Marathon, Awards & Expo za mwaka 2022.
Rc Mwasa amesema Tuzo hiyo ni ishara ya kutambua nafasi ya TAHA katika kuendeleza sekta ya horticulture nchini hasa huduma za masoko, mazingira wezeshi ya biashara, huduma za ugani ili kuongeza tija na ubora, kuongeza thamani mazao.
Katika tamasha Hilo pia Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA Jacqueline Mkindi ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo za Kilimo Marathon, Awards and Expo za Mwaka 2022 kama Mwanamke Mwenye mchango mkubwa zaidi katika kuendeleza sekta ya Kilimo Nchini.
Tamasha la kilimo marathoni limeandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa Morogoro lengo kwa kishirikina na wadau mbalimbali lengo kuhamasisha wananchi kulima.kilimo chenye tija , utunzaji mazingira samabamba na maandalizi ya msimu mpya was kilimo Mkoani humo huku taasisi mbalimbali Serikali na binafsi zikishiki.