Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji Mkoani Kagera lengo ikiwa ni kuzidi kukuza uchumi wa Mkoa huo na kutoa ajira kwa watu wengi.
Ameyasema hayo wakati akiongea na wahitimu,wanachuo na baadhi ya wananchi waliohudhuria mahafali ya saba ya wahitimu wa Chuo Cha King Rumanyika kilichopo manispaa ya Bukoba,kilichoanzishwa na Mkurugenzi Godson Gypson Rwegasira ambaye pia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba.
Awali mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba Gypson Rwegasira ameseama kuwa pamoja na kozi nyingine wameamua kuunga mkono juhudi za Rais Samia upande wa elimu ambapo wameanzisha mpango maalumu wa kufadhili sehemu ya gharama za mafunzo kwa walimu wa shule za msingi waliopo kazini ambao wanajiendeleza kwa upande wa (Diploma) wanasomeshwa kwa mchango wa chuo hicho kwa kushirikiana na baadhi wa wabunge wa majimbo yaliyopo Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa Mwassa amepongeza jitihada hizo huku akiahidi kuendelea kuwa nao karibu ili kuhakikisha wanazidi kufanya vizuri na kuwasaidia vijana wa Kitanzania kupitia Elimu huku akiwashauri wahitimu kutumia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Rais Samia ili waweze kujikwamua kiuchumi.